Meneja
wa klabu ya soka ya Manchester United sir Alex ferguson amewataka
wachezaji wake kuwa uhuru zaidi katika mechi za ligi kuu ya soka ya
nchini Uingereza zilizosalia msimu huu kwani tayari wameshatwaa ubingwa
wa 20 katika historia ya michuano hiyo.
Licha ya ubingwa wa mapema waliojinyakuliua, Ferguson amewasihi
wachezaji wake kuwa makini na kulinda heshima waliyojiwekea msimu huu
wakati watakapokutana na Chelsea katika dimba la Old Trafford jumapili
hii.
United watacheza bila mshambuliaji wao Danny Welbeck ingawa kumekuwapo na taarifa kuwa kiungo Paul Scholes aliyekuwa akikabiliwa na majeraha ya goti toka mwezi January yupo tayari kushuka dimbani kwa sasa.
Manchester United sasa wanasubiri kombe lao la ligi kuu watakalokabidhiwa tarehe 13 ya mwezi huu ambayo itakuwa ni siku moja tu baada ya mchezo wao mwisho na Swanse
a kwenye dimba la nyumbani la Old Traford siku ya tarehe 12 mwezi huu.