Jumapili, 5 Mei 2013

WATU WATATU WAMEKUFA KATIKA MLIPUKO WA BOMU KANISANI ARUSHA

Takriban watu watatu wamekufa kwenye mripuko wa bomu Jumapili asubuhi katika kanisa Katoliki la Olasiti nje kidogo ya mji wa Arusha, Tanzania.engine kadhaa walijeruhiwa huku balozi wa papa na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya kuzindua parokia mpya ya mtakatifu Yosefu walinusurika.
Kwa mujibu wa Padri Festus Mangwangi ambaye ni paroko msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la Arusha, mripuko ulipotokea walikuwa tayari kubariki maji kwa ajili ya uzinduzi wa kanisa, shughuli iliyokuwa ikiongozwa na balozi wa Papa Francis.


Hata hivyo Padre Mangwangi ameiambia BBC kuwa taarifa walizonazo muda mfupi baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali, kuna watu watatu kati yao waliofariki na wengine wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru mjini Arusha
 
Taarifa moja inasema watu kama 80 walijeruhiwa.
Watalaalamu wa miripuko na polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na mlipuko huo.
Bado hakuna taarifa ya chanzo cha mripuko au kama kuna mtu au kundi lilohusika.
Lakini msemaji wa polisi alieleza kwamba wanashuku kuwa mripuko ulisababishwa na bomu.


Kwa mujibu wa Radio Free Afrika zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa katika mlipuko huo ambao polisi wanaendeleo kufanya uchunguzi wa kina.






Hili ni shambaulio la kwanza la bomu nchini Tanzania japokuwa mwaka huu pia kulikuwa na tukio la mauaji ya Padre wa kanisa hilo visiwani Zanzibar, ambaye alipigwa risasi wakati akiwa anajiandaa kuingia kanisani. Chanzo: www.bbcswahili.com na Radio Free Afrika.