Manchester United imemtangaza David Moyes aliyekuwa anainoa
Everton kuwa ndiyo kocha mpya wa Mashetani hao Wekundu ambapo atasaini
mkataba wa miaka sita ifikapo tarehe mosi ya mwezi Julai.
Sir Ferguson ndiye alitangaza kufikiwa kwa makubaliano baina ya Bodi ya Wakurugenzi wa Manchester United na Moyes ili aweze kuwa mrithi wake hapo Old Trafford kunzia msimu ujao.
Moyes mwenye umri wa miaka 50 anaondoka Goodison Park baada ya kuifundisha Everton kwa kipindi cha miaka 11 bila ya kuipa taji lolote huku kitu pekee ambacho anasifiwa kukifanya na kutengeneza kikosi imara.
Sir Ferguson ndiye alimpendekeza Moyes kuwa mrithi wake ambapo mwenyewe amemsifu ni kocha imara mwenye vigezo vyote vinavyopaswa kuweza kuinoa Manchester United kwa siku zijazo.
Moyes mwenyewe baada ya kutangazwa kuwa mrithi wa Sir Ferguson amekiri hiyo ni heshima kubswa ana kwake na anashukuru kwa kupewa kazi hiyo na ameahidi kuhakikisha anailetea mafanikiwa Manchester United.
Klabu ya Everton imetoa taarifa yake ya kumshukuru Moyes kwa kazi aliyoifanya kwa kipindi cha miaka 11 aliyokuwa anaifundisha timu hiyo huku wakimtakia kila la kheri katika kazi yake mpya.
Beki wa Kati wa Manchester United Rio Ferdinand ni miongoni mwa waliouzungumziaujio wa Moyes ambapo yeye amesema kuna vitu ambavyo analingana na Sir Ferguson hivyo ana imani atakuwa na mafanikio Old Trafford.