 |
, Yousuf Raza Gilani, Ali Haider Gilani ambaye ametekwa na watu wenye silaha |
Watu
wenye silaha nchini Pakistan wamemtekanyara mtoto wa Waziri Mkuu wa
zamani wa taifa hilo Yousuf Raza Gilani, Ali Haider Gilani katika siku
ya mwisho ya kampeni kabla ya wananchi wa Taifa hilo hawajapiga kura
siku ya jumamosi.
Haider Gilani ametekwa katika Mji wa Multan baada ya kuzuka
mashambulizi kwenye kampeni zake za mwisho na ndipo watu hao walimteka
na kwenda naye kusikojulikana hadi sasa.
Familia ya Waziri Mkuu wa zamani Raza Gilani imekuwa na nguvu kubwa
katika Chama cha Watu wa Pakistani PPP na wamekuwa wakisimama kidete
kuhakikisha wanashinda viti vya kutosha Bungeni.
Kampeni za Chama cha PPP zilishapewa kitisho kutoka kwa Wanamgambo wa
Taliban ya kwamba zitashambuliwa lakini hakuna hatua zozote madhubuti
zilizochukuliwa kujikinga na tishio hilo.
Licha ya Wanamgambo wa Taliban kutoa kitishi hicho mapema lakini
halijajitokeza na kuthibitisha iwapo linahusika na utekajinyara wa
Haider Gilani kipindi hiki msako ukiendelea kufanywa.
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Raza Gilani kwa upande wake ametupa
lawama kwa wapinzani wake kisiasa ambao anaamini wapo nyuma ya tukio
hilo kwa kuliandaa na hatimaye kulitekeleza.
Raza Gilani ambaye mahasimu wake wa kisiasa wamekuwa wakitumia kila
mbinu kuhakikisha wanamdhoofisha kisiasa lakini yeye ataendelea
kukabiliana nao kwa njia zozote zile.
Afisa wa Polisi Khurram Shakur amewaeleza wanahabari watu
wwaliojihami kwa silaha walifika na kushambulia mkutano huo siasa na
kisha kumteka Haider Gilani na kutoroka naye kwenye gari jeusi.
Kaka yake Haider Gilani, Ali Musa amesema wanataka Jeshi la Polisi
kufanyakazi yake ipasavyo na kuhakikisha ndugu yao anapatikana haraka
iwezekanavyo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi siku ya jumamosi.
Duru za usalama zinasema mtu mmoja alipoteza maisha kwenye shambulizi
hilo lililochangia utekwajinyara kwa Haider Gilani na tayari familia
yake imetaka Jeshi la Polisi kuhakikisha kijana wao anapatikana akiwa
hai.
Kundi la Wanamgambo wa Taliban limeshatishia kufanya mashambulizi
siku ya uchaguzi huo ambao utafanyika siku ya jumamosi wakisema hawataki
kufanyika kwa uchaguzi huo uliowatenga wao.