Hatimaye
watu Kumi wanaodaiwa kumuua Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba,
Sengondo Mvungi Jana walifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Dar es salaam, wakikabiliwa na kosa Moja tu la kumuua Dk.Mvungi kwa
kukusudia.
Wakili wa serikali Aida Lusumo Mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo
aliwataja washitakiwa Hao Kuwa ni chibago Magoze (32),John
Kanjunju(29),John Mayunja,Longishu Losingo(29),''Masunga Makunza,Paulo
Dondondo(30),mkanda Mlewa(40),zakaria msese(33),msungwa Matonya(30) na
Ahmed kilebu(30).
Wakili Lusumo alidai wanashitakiwa kwa kosa la Kua kwa kukusudia
kinyume na kifungo Cha 196 Cha Sheria ya kanuni a adhabu ya Mwaka 2002 ,
Kuwa Novemba 11 Mwaka 2013 huko eneo la msakuzi kino done Dar es
salaam, wote kwa pamoja walimuua Dk.Mvungi ambaye alikuwa ni mhadhiri wa
Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es salaam na kwamba upelelezi bado
haujakamilika.
Hakimu Fimbo aliwataka washitakiwa Hao wasiyonaidai chochote kwasababu
Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza Kesi hiyo hivyo akaamuru
washitakiwa wapelekwe gerezani.
Washitakiwa walifikishwa chini ya Ulinzi MKALI wa wanausalama AMBAPO
walipandishwa Kwenye Gari aina ya Landcruser yenye namba za usajili KX
06EFD na walisikikiza na Gari aina ya Noah yenye namba za usajili T 539
CCB ambalo Lilikuwa likiongoza msafara huo.
Chanzo:Tanzania Daima la Jumamosi ,Novemba 23 Mwaka 2013