Meya
wa jiji la Toronto nchini Canada, Rob Ford amekiri kutumia dawa za
kulevya aina ya cocaine lakini amesema hatajiuzulu nafasi yake hiyo ya
uongozi kwa kuwa ameshaomba msamana na haya ni mawimbi tu yatapita.
Kwa miezi kadhaa Meya huyo alikuwa akipinga habari ziliripotiwa kuhusu tuhuma za yeye kubwia dawa za kulevya, taarifa ambazo zilionekana kufifia nguvu na pengine kufa hadi siku ya Alhamisi ya wiki hii, pale Chifu wa Polisi wa Toronto, Bill Blair aliposema kuwa walikuwa wakifanya uchunguzi ambao asa umewawezesha kupata video isiyo na tashwishi ikimwonesha na

kuthibitisha
kwa picha kuwa Ford ndiye mhusika aliyetajwa kwenye ripoti hizo na
matukio ya kwenye video hiyo yanalandana na ripoti zilizotolewa kwenye
mitandao mbalimbali.
Wakili wa Ford anapinga kwa kusema kuwa video husika haimwoneshi mteja wake akibwia unga.
Jumapili, katika kipindi cha redio kwenye kituo cha 1010 ambacho kinaendeshwa na Ford na kaka yake, Ford amemwambia Chifu wa Polisi airuhusu video hiyo ionekane kwa umma kwa kuwa wakazi wa Toronto wana haki ya kuiona na kuhukumu.
Video hiyo iliripotiwa kwanza na gazeti la Star na tovuti ya Gawker ambao wao walisema walioneshwa tu video hiyo katka nyakati tofauti na mtu aliyetaka kuwauzia ili waitumie kwa ajili ya habari, hivyo Gawker wakakusanya fedha na kuinunua na baadaye wakasema hawawezi kumtambulisha mtu aliyewauzia video hiyo kwa kuwa hawana mawasiliano naye tena.
Chifu wa Polisi, Blair yeye alisema waliipata video hiyo wakati wakichimbua kifa cha kompyuta, yaani 'hard drive' iliyokuwa imefutwa ili kuficha ushahidi wa dawa za kulevya.
Ford mwenyewe hakuzungumzia kuhusu kilichomo kwenye video hiyo akidai kuwa ilikuwa inahusika na uthibitisho wa madai ya tukio jingine ambalo kesi yake ipo mahakamani.
Ford ameomba msamaha kwa makosa ambayo hakuyaweka wazi. Alisema, “Mimi ni wa kwanza kukiri, rafiki, mimi ni wa kwanza kukiri, kuwa si mkamilifu. Nimekosa… na ninaloweza kufanya sasa ni kuomba msamaha kwa kukosea,” Ford amekaririwa na Reuters akitamka maneno hayo redioni na takriban saa moja baadaye akaongeza, “Nimekosea. Sijui nianzia wapi? Kwa mfano pale Danforth, ule ulikuwa ujinga kabisa. Sikupaswa kuwa-nzwiii pale Danforth. Kama umepanga kwenda kunywa chupa kadhaa za pombe, unapaswa kukaa nyumbani, basi. Huendi mbele ya kadamnasi na kujifanya shujaa mbele ya hadhara. Ninaomba msamaha kwa dhati kabisa, kwanza kwa familia yangu, pili kwa raia na tatu kwa walipa kodi wa jiji hili kubwa. Hakika siwezi kubadili yaliyopita, kilichobakia ni kusonga mbele na kujifunza kutokana na makosa na ninakuhakikishieni nimejifunza”
Reuters inasema, ikiwa unadhani kuwa sakata hili limeongoa imani ya wapiga kura kwa Ford, utakuwa umekosea kwani kituo cha CBC kimeripoti kuwa matokeo ya kura za haraka haraka yanaonesha kukubalika kwa Ford kumeongezeka kwa asilimia 5 na kufikia 44%.