Waathirika wa kesi inayomkabili rais wa Kenya, Uhuru
Kenyatta wameutaka Umoja wa Mataifa kukataa wito wa kutaka
kucheleweshwa kwa kesi dhidi ya Rais Kenyatta katika mahakama ya
kimataifa ya ICC mjini The Hague, Uholanzi.
Baadhi ya viongozi wa Afrika wameandaa rasimu ya
azimio la kuomba kesi inayomkabili Rais Kenyatta iahirishwe kwa mwaka
mmoja kwa masilahi ya usalama wa taifa, kufuatia shambulio la kigaidi
katika kituo cha kibiashara cha Westgate mjini Nairobi.Lakini mwanasheria wa waathirika, Fergal Gaynor, amesema kucheleweshwa kwa kesi kutapunguza nafasi ya kupatikana haki kwa waathirika. Bwana Kenyatta anakanusha mashitaka yanayomkabili dhidi ya uhalifu wa kibinadamu, kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.