Jumanne, 30 Aprili 2013

GOD BLESS LEMA APEWA DHAMANA


subuhi ya Jumatatu, kama ilivyotarajiwa na wengi baada kufuatia taarifa mbalimbali katika v

yombo vya habari, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa Arusha baada ya kukaa rumande tangu alipokamatwa usiku wa kumkia siku ya Jumamosi, Aprili 27, 2013.                               

  HIVI NDIVYO ALIVYO SOMEWA SHITAKA

Mbele ya hakimu Devotha Msofe na mawakili Kimomogoro na Humphrey Mtui wanaomtetea, Lema amesomewa shitaka la kosa la uchochezi linalomkabili kwamba aliwachochea wanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha kumzomea Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuwaambia wanafunzi kuwa Mkuu huyo wa Mkoa, “hajui chuo cha uhasibu kilipo, amekuja akiwa amechelewa na anaingia hapa kama anaingia kwenye send off.”

 LEMA AKANA SHITAKA

Hata hivyo, mtuhumiwa Lema amekana kosa hilo. Mwendesha mashitaka alisema dhamana ipo wazi kwa mtuhumiwa endapo atatimiza masharti ya dhamana.

ATIMIZA MASHARTI YA DHAMANA

Mtuhumiwa alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwepo kwa mtu mmoja mwenye kitambulisho kinachokubalika kisheria na kuweka rehani kiasi cha shilingi milioni moja.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 29 Mei mwaka huu.

BAADA YA DHAMANA

Baada ya kutoka mahakamani hapo, Lema alielekea k
wenye maeneo ya Ofisi za chama, CHADEMA.

Chanzo:www.wavuti.com