Jumamosi, 15 Juni 2013

HONGERA SANA MWANADADA LADY JAY DEE KWA KUFANYA BONGE LA SHOO NYUMABANI LOUNGE ANGALIA PICHA HIZI HAPA.

 ndani mambo yalikua hivi

Hivi ndivyo hali ilivyokua ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam ambapo jana usiku kulikua na bonge moja la show la Mwanadada mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hii wanamuziki mbali mbali walipanda jukwaani akiwepo Mh. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.

 Wadau mbali mbali wa muziki hapa nchini wapo ndani ya ukumbi huu hivi sasa kusuhudia show hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki.

 Ndani ilikua nyomi la hatari,lakini nje nako watu bado walikua wanataka kuingia huku wengi wao wakisema kuwa "hata kama hakuna siti,sie tuko radhi kusimama ilimradi tumsapoti Dada yetu".

 Getini mambo yalikua namna hii.

 Foleni ilikua ni ndefu na watu bado walizidi kuingia ukumbini.

Facebook Blogger Plugin by 2jiachie