Headlines News :
Mwanafunzi wa Chuo kikuuu cha Dodoma, ndugu Justice Donatus amefanikiwa kutengeneza mtandao wake wa kijamii uitwao MAYOCOO ambao utasaidia kuiunganisha jamii ya kitanzania na kimataifa..
Akiongea na mwandishi wetu mjini
Dodoma, Justice ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika
chuo hicho ameeleza furaha aliyo nayo kwa kutimiza ndoto yake
ya muda mrefu ya kuja na mtandao mpya wa kizalendo ambao
utaipiku mitandao ya kigeni kama Facebook na Twiitter
Mtandao huo ulizinduliwa rasmi
Jumamosi ya wiki iliyopita chuoni hapo chini ya Usimamizi wa
taasisi ya kuendeleza vipaji kwa vijana iitwayo AISEC na tukio
hilo lilidhaminiwa na makampuni mbalimbali ikiwemo bank ya CRDB
Jiunge na mtandao huo hapo chini ili ufaidi matunda ya kitanzania
Juu na chini ni Wadau wa Mayocoo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo
Justice Donatus akizindua mtandao huo
Facebook Blogger Plugin by 2jiachie |