Jumatatu, 29 Julai 2013

WASOMI;Mchawi wetu ni serikari.Mhadhiri ahoji Mwigulu Nchemba kufanya kazi za DPP,DCI

MDAHALO wa kujadili mstakabali wa amani ya taifa ulioandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), umeibua mambo mazito ambapo washiriki wameinyooshea kidole serikali wakidai ndiye mchawi wa wananchi.

Mdahalo huo ambao kauli mbiu yake ilikuwa ni Mustakabali wa Amani na Usalama wa 
Wananchi wa Taifa Letu kwa Miaka 50 Ijayo, ulifanyika jana katika Ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwashirikisha wanazuoni, wanasiasa, viongozi wa vyombo mbalimbali vya ulinzi na serikali.
Wachokoza mada walikuwa ni mhadhiri wa sheria wa chuo hicho, Dk. Onesmo Kyauke aliyegusia mfumo wa utendaji wa Jeshi la Polisi katika kusimamia amani ya nchi, Profesa 
Benadetha Kiliani, mtaalam wa sayansi ya siasa na utawala kwa umma na mwanahabari nguli na mhadhiri wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari, Dk. Ayoub Rioba.
Katika mada yake, Dk. Kyauke aliliponda jeshi la polisi linavyokiuka sheria katika kutekeleza majukumu yake kiasi cha kuruhusu kuingiliwa na wanasiasa na kuelekezwa jambo la kufanya.
Bila kuuma maneno, mhadhiri huyo alimtaja wazi wazi Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Mwigulu Nchemba, akidai kwa sasa analiendesha jeshi hilo kwa kuingilia majukumu ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mwendesha Mashataka Mkuu (DPP).
Alisema kuwa mwanasiasa huyo ambaye ni mbunge wa Iramba Magharibi, amekuwa akiwatuhumu wanasiasa wa vyama vya upinzani kuwa ni magaidi na polisi wamekuwa wakiwakamata na kuwafungulia mashtaka hayohayo anayosema kada huyo bila hata kuwa na ushahidi.
Dk. Kyauke alitolea mfano wa matukio ambayo Nchemba amekuwa akiyafanya kuwa ni pamoja na lile la kuonyesha ushiriki wa kupanga tukio la ugaidi la Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Wilfred Lwakatare.
Tukio lingine alisema ni wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani jijini Arusha, ambapo kiongozi huyo aliwataka wananchi wa jiji hilo kutochagua madiwani wa CHADEMA kwa kuwa ni chama cha ugaidi kwa madai kwamba ndio waliohusika kummwagia tindikali kijana wa CCM kule Igunga.
Kutokana na matamshi hayo, mhadhiri huyo alisema baadhi ya wanachama wa CHADEMA waliweza kukamatwa kama njia mojawapo ya kuisaidia polisi; jambo linalowafanya kama wasomi kujiuliza kuwa Mwigulu siku hizi kawa DCI au DDP?
Kuhusu utendaji wa Jeshi la Polisi, alisema ndilo limekuwa chanzo kikubwa cha uvunjifu wa amani kwa kupoka haki ya Kikatiba ya wananchi kuandamana na kufanya mikutano huku akitolea mfano wa mauaji yaliyofanywa na jeshi hilo ya mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, kijijini Nyororo, mkoani Iringa, wakati wa kuzindua matawi ya CHADEMA.
Katika mauaji hayo, alisema ushahidi wa wazi umeonyesha namna gani polisi walivyoshiriki na tume zote zilizoundwa zikamuelekezea kidole Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa na Msajili wa Vyama vya Siasa, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa hadi leo zaidi ya polisi mwenye cheo kidogo akitolewa kafara huku mkubwa wake akiendelea kupandishwa cheo.
Pia alisema kumekuwepo na upendeleo wa jeshi hilo kwa kutetea chama tawala ikiwemo enzi za IGP Omar Mahita kudai kuwashikilia wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) na majambia ingawa hadi leo wamekosa uthibitisho lakini kutokana na uongo huo wameshindwa kumchukulia hatua kiongozi huyo.
Katika mapendekezo yake, Kyauke aliitaka polisi kubadili mfumo wake wa kufanya kazi, na kuhoji kwa nini Tanzania ni dhambi kuandamana huku akimtaka Waziri Mkuu kufuta kauli yake ya kutaka wananchi kupigwa tu na jeshi hilo wanapokaidi amri.
Prof. Kilian kwa upande wake, alisema mpaka sasa bado kiini cha uvunjifu wa amani hakijagundulika na badala yake pande zote zimekuwa zikirushiana mpira ikiwemo serikali, wananchi na wanasiasa.
Alizitaja sababu zinazochangia matukio hayo kuwa ni pamoja na hali ya upinzani kuja juu hivyo chama tawala kinajihami kutokana na mabadiliko hayo, kuongezeka kwa kiwango cha umaskini na mfumo wa kiliberali ambao umechangia matabaka na uhuru wa kutoa maoni tofauti na enzi za ujamaa.
Naye Dk. Rioba alisema suala la amani sio la kuombewa kanisani au msikitini bali ni la kisayansi zaidi na kudai kwamba wanasiasa wamekuwa wakijidanganya pale wanapowahimiza watu kuliombea taifa liwe na amani.
Pia Rioba alikanusha vyombo vya habari kuwa vimekuwa vikichangia kuharibu amani na badala yake alivifananisha vyombo hivyo na bunduki ambapo kama isipotumiwa kamwe haiwezi kuharibu amani.
Akifafanua hili alisema vyombo vya habari vitaharibu amani endapo tu wanasiasa watavitumia na kuitaka jamii ielewe kwamba vyombo hivyo vina dhima kubwa kama mlinzi wa taifa na ndio maana wakati mwingine vinapendekezwa kuwa NGO’s ili viweze kufanya kazi kwa uhuru zaidi.
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa alisema mchawi wa hayo yote ni serikali, huku akinukuu ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyomtuhumu aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, na Msajili wa Vyama vya Siasa. Akisema amani sio suala la kuhubiriwa au kujadiliwa bali ni matokeo ya utekelezaji wa haki mbalimbali.
Slaa pia alilalamikia vitendo vya ukatili vilivyofanywa Mtwara na vyombo vya dola dhidi ya wananchi, huku akimnyooshea kidole Brigedia Elia Athanas aliyekuwa amemwakilisha Mkuu wa Majeshi.
“Jeshi letu lilikuwa linaheshimika sana, lakini siku za hivi karibuni linaelekea kupoteza heshima yake kwa jamii, tukirejea mfano katika uchaguzi mkuu uliopita ambapo mnadhimu wa jeshi, Abdulrahman Shimbo, alivyotoa kauli yenye utata, jeshi linaingiaje kwenye siasa wakati suala la uchaguzi ni suala la kiraia?” alihoji.
Hoja ya Dk. Slaa kuhusu utendaji wa jeshi la wananchi mkoani Mtwara ilipingwa kwa haraka na Brigedia Athanas akisema: “Naomba kuweka wazi kuwa jeshi letu liko Mtwara, lina adabu na vitendo ambavyo vimekuwa vikiripotiwa ni vya propaganda tu kama alivyosema Dk. Slaa.”
Licha ya kiongozi huyo kujitetea, mchangiaji aliyefuata, Julius Mtatiro ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Tanzania Bara), alithibitisha kuwa wanajeshi wanabaka na walitenda vitendo vya kikatili dhidi ya raia na viongozi wa chama hicho akiwemo mkurugenzi wao, Shaweji Mketo.
Mwakilishi wa NCCR Mageuzi, Faustine Sungura, alisema chama hicho hakiko tayari kufanya maandamano bali kinapambana kwa nguvu ya hoja na kwamba wataendelea kutumia nguvu ya hoja.
Akihitimisha kongamano hilo, Wazri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema kuwa kati ya mambo ambayo yanampa changamoto ni amani ya nchi hii.
“Tulirithi nchi ikiwa na amani, hivyo tuna deni la kurithisha nchi hii ikiwa ya amani katika kizazi kijacho.
Dk. Nchimbi alikemea suala la udini, akiwatahadharisha Watanzania kuwa wasiingie katika vurugu na wasikubali kugawanywa kwa sababu ya dini zao.
“Tukiingia katika vurugu za dini hatutapona, Wakristo na Waislam wote tukatae kugawanywa kwa kutumia misingi ya udini kwa manufaa ya Tanzania ya sasa na kizazi kijacho.
Waziri Nchimbi huku akimtambua Dk. Slaa, alisema wanasiasa wote wana wajibu wa kuwatumikia wananchi, “Suala la amani sio suala la Chama cha Mapinduzi peke yake, ni suala la wanasiasa wote wa chama tawala na wapinzani kutambua kuwa wao ni watumishi wa umma, na kuvumiliana kisiasa ndiko kunaleta amani.

RC, RPC Arusha wawakana FBI


Arusha, Habari na MTANZANIA Jumapili,Picha na 2jiachie.
MKANGANYIKO wa taarifa za ushiriki wa Makachero wa Taasisi ya Kijasusi ya Marekani (FBI), katika uchunguzi wa mlipuko wa bomu katika Viwanja vya Soweto, jijini Arusha, sasa umechukua sura mpya,
Ikiwa ni takribani mwezi mmoja na siku 13 tangu mlipuko huo utokee kwenye mkutano wa Chadema wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani, viongozi waliowahi kuthibitisha juu ya ushiriki wa makachero hao wa FBI kwenye uchunguzi wa tukio hilo sasa wameanza kukana matamshi yao.
MTANZANIA Jumapili lilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, ambaye mwanzoni mwa mwezi huu alikaririwa na chombo kimoja cha habari (si Mtanzania) akithibitisha ushiriki wa FBI katika upelelezi huo, alikana kuwahi kuzungumza juu ya taarifa hizo.

Juni 12 mwaka huu, gazeti hilo lilimkariri Sabas akisema: “Tunaendelea na uchunguzi wa kina mlipuko wa bomu Soweto, tayari wenzetu wa FBI na polisi wa Kenya wamefika kushirikiana nasi, nachukua fursa hii kuwaomba wenye ushahidi utakaosaidia upelelezi kujitokeza”.
Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, Kamanda Sabas alisema, hajawahi kutoa taarifa kama hizo.

“Watu wanatoa wapi hizo taarifa, mimi sijawahi kutoa taarifa hizo,” alisema Kamanda Sabas.

Kuhusu watu waliodaiwa kushikiliwa kutokana na mlipuko huo wa bomu, Kamanda Sabas alisema kwa sasa wapo nje kwa dhamana, kutokana na upelelezi wa tukio kuendelea.

“Ikifikia hatua ya kujulishwa nitawaita kwa sasa bado tunaendelea na uchunguzi,” alisema Kamanda Sabas.

Wakati mkanganyiko huo wa FBI ukionyesha kuchukua sura tofauti, taarifa za vyombo vya habari zimewahi kuunukuu Ubalozi wa Marekani nchini ukikana kuwapo kwa wapelelezi wake jijini Arusha kuchunguza tukio hilo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, alipoulizwa juu ya taarifa za kukanganya za ushiriki wa FBI kwenye tukio hilo la bomu, alijibu kwa kifupi; “Tafuta watu wanaofanana na swali hilo.”

Hata hivyo, Mwandishi wa habari hizi alipomueleza kwamba ameulizwa swali kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Arusha, Mulongo alisema; “Hakuna kitu kama hicho.”

Akiwa katika cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC), Mulongo aliwaambia wajumbe wa kikao hicho kuwa taarifa za awali kutoka kwa makachero wa polisi nchini zimebaini mtandao wa ulipuaji mabomu jijini Arusha, ulipangwa ndani ya jiji hilo.

Mulongo alisema mbinu hizo zilijulikana kutokana na wananchi waliojitokeza kuwasilisha ushahidi kwa vyombo vya dola ambapo mpaka wakati huo ushahidi ulionyesha mtandao wa waliolipua mabomu hayo ulianzia jijini Arusha.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema kuwa Jeshi la Polisi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha waliwadanganya Watanzania kuwa Makachero wa FBI wanakuja kuchunguza tukio hilo wakati si kweli na Ubalozi wa Marekani ulikanusha suala hilo.

Mbowe alisema kauli kama hizo zimekuwa zikitumika kuwahadaa Watanzania.

Juni 15, mwaka huu, katika viwanja vya Soweto, CHADEMA wakiwa kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani, bomu lililipuka na kuua watu wanne na kujeruhi takribani 70.

Tukio hilo liliibua hisia nyingi na wakati fulani kulazimu maofisa wa Jeshi la Polisi Makao Makuu Dar es Salaam kwenda jijini Arusha kufuatilia kwa kina ambapo baadaye ilielezwa kuwa FBI wametua jijini humo ili kubaini ukweli.

Tangu kutokea kwa mlipuko huo, kumekuwa na mvutano mkubwa baina ya Jeshi la Polisi na Chadema, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho kuueleza umma kwamba wanao ushahidi wa polisi kuhusika kwenye tukio hilo, huku akigoma kuwasilisha ushahidi.

Mbali na bomu la Soweto, bomu jingine lilirushwa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti na kusababisha watu watatu kufariki ambapo upelelezi wake nao unatajwa kuendelea kufanywa.
Habari na MTANZANIA Jumapili

MSHIRIKI WA TANZANIA (NANDO ) ATIMULIWA BIG BROTHER BAADA YA KUGOMBANA NA MSHIRIKI MWENZAKE.


Nando  ametimuliwa  katika  shindano  la  big  brother  baada  ya  kugombana  na  mshiriki  mwenzake  Elikem wa Ghana  siku  ya  ijuumaa  ya  tarehe 26/7/2013...

Hii  ni  ripoti  ya  DSTV ikisimulia  sakata  hilo.
-----
After tonight's Evictions that saw Annabel and Sulu being given the boot, Big Brother then gathered all of the Housemates in the living room.

Today Big Brother reproached Nando for the fight that he had with Elikem on Friday. The heated face-off with Elikem saw the two fellas exchanging fiery words between them. Nando is the one that instigated the fight. Instigation and provocation is a violation of the Big Brother rules.

"Any Housemate who becomes physically violent will be removed from the House immediately. Violence can refer to self-inflicted violence, or violence towards another. Violence includes provocation, goading, bullying and victimisation," said Biggie.

This season Big Brother has imposed a Three Strike Rulu, which will be applicable to Housemates who commit serious infringements.

 For this fight Nando received his second Strike and Elikem was has served with his first Strike. Afterwards the Tanzanian was called into the Diary Room. He was given his third Strike for making threats against Elikem's life, saying: "I feel like stabbing him. A nigga like that deserves to die".

And he was also caught sleeping with scissors under his bed and this is not the first time that he has been caught with a weapon in the House. The troubled young fellow has had a dramatic nine weeks in The Chase.

 Last month he was served with a a Strike and a stern warning from Big Brother after he was found carrying a knife to the Channel O Party. The possession of weapons or intention to be violent in the House is another violation of the Big Brother rules.

After the Diary session Nando was told to immediately exit the House. Big Brother then gave a warning to the Housemates to conduct themselves as adults.
Facebook Blogger Plugin by 2jiachie | 2jiachie

Ijumaa, 26 Julai 2013

CHELSEA YAIFUNGA INDONESIA ALL STAR 8-1

Marco Van Ginkel, Gary Cahill na John Terry wakijumuika pamoja kushangilia baada ya kuifunga timu ya Indonesia All Stars
All smiles: Jose Mourinho watches as his side stroll to an easy win in Jakarta
Jose Mourinho kwenye benchi akiangalia timu yake ikigawa dozi kiurahiisi mjini Jakarta
Going wild: Fans in Indonesia celebrate as Chelsea thrashed the All-Stars
Mashabiki waliovalia jezi za Chelsea wakishangilia uwanjani Baada ya kuona mvua ya mabao kwa Indonesia All Stars
Captain: Chelsea's John Terry (right) celebrates scoring his side's fourth goal of the game with teammates
Kapten John Terryakishangilia na wenzake
No mistake: Chelsea's Eden Hazard scores his side's first goal of the game from the penalty spot
Eden Hazardakifunga bao la penati dakika ya 22 na kuifungulia Blues Mvua ya Mabao leo
Just warming up: Demba Ba (left) and Ramires celebrate the Blues going 3-0 up
Demba Ba na Ramires wakiitimisha jumla ya mabao 3-0
Easy: Chelsea's Ramires (second right) celebrates scoring his side's second goal of the game with teammates
Ushindi mtamu jamani!!!
Through the paces: Chelsea's second half team warmed up at the tail end of the first 45 minutes
Dalili za Ushindi kwa Chelsea zilionekana mapeema katika kipindi cha dakika 45 za kipindi cha kwanza
KIKOSI CHA CHELSEA:
Chelsea: Blackman (Schwarzer 46); Wallace (Ivanovic 46), Cahill, Terry (Kalas 46), Bertrand (Cole 46); Chalobah (Essien 46), Van Ginkel (McEachran 60); Ramires (Feruz 60), Hazard (Piazon 60), Moses (Traore 46); Ba (Lukaku 46).

Goals: Hazard (penalty) 21, Ramires 29, 56 Ba 32, Terry 45, Traore 50, Lukaku 52, 65.

Indonesia All-Stars goal: Kalas (og) 67

CREDIT : BUKOBA SPOTS
Facebook Blogger Plugin by 2jiachie | 2jiachie

MATUKIO YOTE YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA WILAYANI MULEBA SIKU YA JANA.


Rais Kikwete aliongoza watanzania Nchini kuhudhuria maadhimisho ya mashujaa waliopigania vita vya ukombozi dhidi ya majeshi ya uvamizi ya Nduli Idd Amini mwaka 1978/79, maadhimisho yaliadhimishwa katika kambi ya jeshi JWTZ Kaboya wilayani Muleba.

Viongozi mbalimbali

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka ngao/sime katika mnara wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera siku ya jana.


Photo: MAADHIMISHO YA MASHUJAA MWAKA 2013 KITAIFA KABOYA
www.bukobasports.com

Viongozi wa dini wakisoma dua kwenye maadhimisho hayo. Pembeni ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Jaji Mkuu Mheshimiwa Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman Makungu




Rais Jakaya Kikwete akitembelea makaburi ya mashujaa waliopoteza maisha wakati wa vita na Nduli Iddi Amini wa Uganda.

Photo: MAADHIMISHO YA MASHUJAA MWAKA 2013 KITAIFA KABOYA MKOANI KAGERA
www.bukobasports.com





PICHA NA HABARI KWA HISANI YA BUKOBA SPORTS.COM
Facebook Blogger Plugin by 2jiachie | 2jiachie

ANGALIA MAPOKEZI ALIYOPATA POKELLO BAADA YA KUREJEA KWAO ZIMBABWE

Baada ya kuwa evicted na kuaga rasmi shindano la Big brother the chase,Qeen of swag Pokello Nare kutoka nchini Zimbabwe hatimaye atua rasmi kwenye ardhi ya nchini kwao na kupata mapokezi ya nguvu katika uwanja wa ndege wa kimataifa Harare.
Mapokezi yakiongozwa na fans wake (team Pokello),familia na aliyekuwa mshiriki mwenzake kutoka Zimbamwe Hakeem Mandaza, Pokello alishindwa kuzuia machozi kwa sapoti walioonesha uwanjani hapo. Pia mtoto wake Gerald (10) alikuwa mmoja wa waliojitokeza ku show love. Baadae alielekea hotelini na gari nyeupe ya kifahari,cheki picha chini zikionyesha mapokezi hayo.

CREDIT: MAMAFRIKA
Pokello akiwa Harare international airport 
Umati uliojitokeza
Team Pokello
Pokello na mtoto wake Gerald

Pokello fan

Pokello akielekea hotelini.
Plugin by 2jiachie | 2jiachie

Jumatatu, 15 Julai 2013

WITO WA KUSITISHA TOZO/KODI YA LAINI YA SIMU KILA MWEZI KUFUATIA MABADILIKO YA SHERIA YA KODI 2013

Sisi wananchi wa Tanzania:
• Tukiwa ni wapiga kura wa majimbo mbalimbali nchini Tanzania, tumechukua jukumu leo kutoa wito kwa wabunge na serikali kufuta tozo/kodi mpya ya laini za simu iliyoanza kutumika baada ya sheria kupitishwa na Bunge Juni 2013.
• Hii ni sehemu muhimu ya wajibu wetu kama raia waaminifu, wenye nia njema ya kuchangia mawazo bora yatakayotuletea maendeleo endelevu nchini kwetu.
• Bila mjadala mpana na mawazo chanya yaliyochambua masuala kwa undani kama msingi wa maamuzi, nchi itafanya maamuzi dhaifu yasiyosimama kwenye misingi ya hoja na ukweli wa mambo.
• Kukaa kimya kwenye jambo ambalo tunaliona linakandamiza wananchi na huenda likaturudisha nyuma kimaendeleo, ni kushindwa kuwajibika kama wananchi.

Tunapinga kodi ya laini za simu
KWA SABABU:- Sisi wananchi hatujashirikishwa kupitia mjadala wa Bunge kuhusu kodi hii kwani Waziri wa fedha hakusoma hiki kipengele wakati wa hotuba yake na tulikosa taarifa mpaka baada ya kupitishwa kwa sheria ya kodi hii.

KWA SABABU:- Kodi hii inamkandamiza mtanzania wa hali ya kawaida na wa hali ya chini ambao ni 67% ya wananchi wanaoishi chini ya kipato cha dola 1.25 (shs 2,000) kwa siku. Takwimu zinaonyesha kuwa kati wa wamiliki wa laini za simu milioni 22, milioni 8 wanatumia chini ya shilingi 1,000 kwa mwezi. Kuwaongezea mzigo wananchi hawa kwa kiwango ambacho tayari wanashindwa kumudu ni kuwanyima kabisa fursa ya kutumia huduma hii muhimu.

KWA SABABU:- Kodi hii haifuati misingi ya kulipa kwa kadri ya matumizi na ni kodi kandamizi inayowatoza wamiliki wa laini ya simu wote kiasi kimoja bila kuzingatia kiwango cha matumizi. Hii inamkandamiza mwananchi wa hali ya chini kwa kumlazimisha kulipa kiwango kikubwa cha kodi kulingana na mapato yake. Tukichukulia mfano wa mtu anayetumia shilingi laki tano kwa mwezi kama muda wa maongezi na yule anayetumia shilingi elfu tano - na tukilinganisha uwiano wa malipo haya na matumizi yao – basi yule anayetumia shilingi laki tano analipa 0.2% ya matumizi yake, ila yule anayetumia shilingi elfu tano anatozwa 20% ya matumizi yake.

KWA SABABU:- Kodi hii ni juu ya ongezeko la kodi mbalimbali katika huduma za simu za mkononi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ushuru kutoka 12% kwenda 14.5% na pia kodi hii kutozwa kwa huduma zote ingawa awali ilitozwa kwa huduma ya matumizi ya kuongea. Hivi sasa utumiaji wa internet, kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu za mkononi unatozwa kodi. Ongezeko hili pekee limeshafanya huduma za simu za mkononi kupanda gharama kwa kiasi kikubwa. Ongezeko hili la shs 1,000 litazidi kuwaumiza wananchi.

KWA SABABU: - Kodi hii pekee inampunguzia mtumiaji muda wa maongezi na huduma zingine za simu za mkononi ikiwa ataendelea na matumizi yake ya mwezi kama kawaida. Kwa mfano mtumiaji akitumia kifurushi cha bei ya shs 475 inayompa dakika 20 za maongezi, 50 MB za data, na sms 100 kwa masaa 24, kwa kodi ya shs 1,000 kwa mwezi ni sawa na serikali kuchukua siku mbili za kifurushi hiki kila mwezi au ni sawa na kuchukua dakika 40 za maongezi, 100MB za data na sms 200 kila mwezi.

KWA SABABU:- Huduma ya simu za mkononi siyo anasa na ni sehemu muhimu ya mawasiliano na kiungo kinachochangia kurahisisha harakati za maendeleo. Kwa mfano wakulima hutumia huduma hizi katika kuuza mazao yao na kupokea fedha; akina mama wajawazito hupelekewa taarifa muhimu kuhusu afya zao; wanafunzi kupitia internet wanaweza kupata habari muhimu zinazohusiana na masomo yao nk. Kodi hii itawanyima fursa ya kutumia huduma hizi muhimu.

KWA SABABU:- Serikali inaweza punguza matumizi yake mengineyo (safari, posho, semina, manunuzi ya magari na kudhibiti ufisadi) hivyo kufidia pengo litakalosababishwa na kusitisha tozo/kodi ya laini ya simu.


KWA SABABU:- Pia, utafiti uliofanywa na Interfaith Standing Committee on Economic Justice and the Integrity of Creation mwaka jana uligundua kuwa kwa wastani Tanzania hupoteza dollar billion moja (takriban shs trilioni 1.8) kila mwaka kutokana na ukwepaji kodi, uhamishaji harama wa fedha na misamaha ya kodi. Tunaitaka Serikali yetu iongeze ufanisi wa kukusanya kodi kutoka vyanzo vilivyopo tayari na kuondoa misamaha kwa hivyo itaziba pengo la shs billioni 264 kutoka kwa kodi ya laini ya simu za mkononi. 
 
Inahitajika sahihi yako ili kupinga sheria ya kulipia laini ya simu ushuru wa shilingi 1,000
                                    BOFYA HAPA KUWEKA SAHIHI YAKO
Credit : www.avaaz.org
 Plugin by 2jiachie